Friday, June 17, 2016

CHOMBEZA KIDOOGO

SEHEMU YA PILI

Unadhani nilifanikiwa kuinua domo langu na kumwambia japo ninakupenda tu? Thubutu! Kila nilipojitahidi kusema sasa nimwambie, ulimi ulikuwa mzito na pale ulipokuwa mwepesi maneno yalifanya mgomo!
Mgomo ulipojisahau yalitoka maneno mengine tofauti kabisa na ninakupenda!

CHOMBEZA KIDOOGO

Kidokezo
…ulikuwa mduara wa Segere kwa lugha isiyo rasmi. Au ‘mnanda’ kama ilivyozoeleka. Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho walikuwa wakizunguka kwa pozi huku wakizungusha viuno vyao taratibu kwa ustadi mkubwa. 
Mirindimo ya ngoma sambamba na kiuno cha mwanamama mmoja kilichokuwa kikizunguka vitamu
vikayafanya macho yangu yamuandame! Yakamwandama kila alipokwenda. 
Halafu ngoma ikazimwa.

NILIVYOSUMBUKA SUMBAWANGA

Ni dunia ya mikiki mikiki. Kuchelewa kufa ni kuona mengi lakini usiombe kukutana na viroja vya Wachawi wa Sumbawanga. Katika kipindi ambacho nimeishi kwenye ulimwengu ambao wengi wanadhani ni wa kufikirika, nimeweza kuuona uchawi na kujua tafsiri yake.Fanya ibada unavyoweza ili wachawi wakae mbali na wewe, vinginevyo utageuzwa chakula kilichoungwa viungo vya kupendeza. Namshukuru Mungu nipo hai, nadunda duniani tena navuta pumzi safi, hewa ya oksijeni. Asante Mungu kwa kunipigania.

CHOZI LA MTOTO JANETH

Kengele ya kutoka darasani iligongwa, wanafunzi wa shule ya msingi wakaanza kutoka madarasani huku wakifukuzana wengine wakipiga kelele ilimradi shwangwe tu.
Ilikuwa mara yangu ya kwanza kufundisha shule za hatua hiyo.
Ilikuwa ni shule ya serikali.
Jicho langu liliangukia katika sura ya msichana mdogo, nguo zake chafu. Alikuwa analia.
Alikuwa peke yake na hakuwa na yeyote wa kumbembeleza.

PENZI LA MAJIVUNO

Juhudi zangu za hapa na pale za kumlaghai binti huyu aingie kwenye himaya yangu ni kama zilikuwa zimegonga mwamba, niliamini kwamba kila neno tayari nimetumia katika kamusi yangu ya longolongo nilizojifunza jijini. Ulikuwa mfadhaiko mkubwa sana yani nilipokuwa mjini haikunichukua muda mrefu sana kumhangaikia msichana sasa hapa kjijini inakuwaje? “Nina mchumba wangu mjini” ndio lilikuwa jibu lake siku zote binti huyu aliyeitwa Ashura bint Zahor, hakuwa na uzuri wa kutisha hata kidogo lakini kwa pale kijijini aliongoza.