Tuesday, August 23, 2016

TANGA RAHA

‘MAMA NINAKUOMBA UNIPE BARAKA ZAKO ILI
NIWEZE KUMUOKOA BABA YANGU’
‘NAKURUHUSU KWA MOYO MMOJA NA MWANANGU
NITAKUPA MSAADA WA CHOCHOTE UTAKACHO
KIHITAJI HATA NUSU YA NGUVU ZANGU NITAKUPA
ILI BABA YAKO AWE HURU KWANI BADO
NINAMPENDA SNA’
‘MAMA NIMEDHAMIRIA KUIANZISHA DUNIA MPYA NA
YENYE KILA AINA YA NGUVU ZITAKAZO IPINGA
MAMLAKA TULIYOPO JUU YETU’
ENDELEA
“Mazungumzo kati ya Hitlaer na mama yake ambaye
ni Janet yaliendelea kwa usiri mkubwa hu-ku mama
yake akimfundisha mbinu ambazo zitamsaidia
mwanae katika kuikamilisha kazi ya kumuokoa baba
yake.Hitler alijipanda vizuri na kutokana ni mjukuu
wa miongoni mwa Malaika wakubwa mbinguni
aliweza kutumia kigezo hicho kushuka duniani bila
ya kuhojiwa maswali mengi na walinzi wanao linda
dunia ambayo ipo katika hali mbaya ya kuuguzwa
moto.

Hitler akaaanza kufanya uchunguzi wake kwenye
shimo kubwa la moto liitwalo KUZIMU lililo kusanya
idadi kubwa ya watu walio tenda maovu,Ila katika
kuzimu nako kumegawanyika madaraja ya mateso
ambayo yapo saba.Na kila waliopo kwenye daraja
moja wanatofautiana kwa adhabu na waliopo kwenye
daraja la pili hivyo hivyo na kuendele mbele kiasi
kwamba ma-tendo yako ndio yanakuchagua uingie
kwenye daraja lipi unalo stahili kuhukumiwa.Hitler
akaendelea kufanya uchunguzi wake katika magereza
yote saba ila hakufanikiwa kumuona baba yake
ambaye kwa jinsi mama yake alivyo muelekeza sio
rahisi kwake kushindwa kumtambua ila gafla Hitler
akiwa kuzimu……”
“Sory Sir Eddy muda wa kipindi chako umeisha”
Madam Zena alizungumza huku akiwa ameshika
vitabu vya somo la Kiswahili jambo lililo pele-kea
wanafunzi kuanza kuzomea wakikataa asiingie
“Jamani tutamalizia hii story yetu kesho”
“Ahhhh Sir EDDY endelea bwanaaa Kswahili bongo
akawafundishe mabasha zakee”
Sauti mmoja ya kiume ikitokea nyuma ya darasa
ilisikika na kumfanya madama Zena kuchungulia
mlangoni huku sura yake ikiwa imekasirika
“Mwana idhaya nani aliye zungumza hayo maneno?”
“Si ninawauliza nyinyi watoto mulio laaniwa na
wazazi wenu.Msio na haya mafirahuni wakubwa
nyinyi munajua maana ya basha……..Ehhhhh au
munavyo jiona nyinyi humu ndani kuna mwanaume
aliye kamilika nyote si mashogaa”
Madam Zena alizidi kutokwa na maneno ya kejeli
hadi ikafikia kipindi wanafunzi wa kiume wa-kaanza
kuzungumza chini chini na neno lililo sikika kutoka
nyuma ya darasa walipo kaa wana-funzi wengi wa
kiume ni
“Shoga baba yako aliyekuzaa”
Nikabaki nimeshika mdomo kwani kwa jinsi madam
Zena alivyo mweupe wa kujichubu taratibu
nikamuona sura yake ikitawali na wekundu kwa mbli
ulio tokana na hasira
“Nasema nyote tokeni nje mupige magoti”
Wanafunzi wote wakakaa kimya wakisikilizia nani
aanze kwenda nje kupiga mogoti ila kadri muda
unavyo zidi kwenda hakuna aliye simama kwenda
nje
“Monitres nenda kamuite Headmaster na mwalimu
wa nizamu”
“MONITRES MSALITIIIIIIIIII”
Monitres baada ya kuisikia sauti hiyo ya wezake
ikambidi akae kwenye kiti chake na kujikausha
kimya na kumfanya madam Zena kuzidi
kuchanganyikiwa na hasira ikazidi kumpanda
“Na wewe Malaya ndio umekataa kunyanyuka kisa
hao washenzi wezako si ndio?”
“Mimi sio Malaya”
“Kama sio umalaya ni nini kinacho kufanya
usiamshe hicho kidude chako uende nilipo kuagiza
kuna mwanaume anaye kupak**?”
Madam Zena akazidi kumfokea mtoto wa watu
ambaye kiumbo ni mdogo sana kiasi kwamba
huwezi kumfananisha na maneno anayoyazungumza
Madam Zena
“Zena hembu kausha basi hawa ni watoto
usizungumze maneno machafu kama hayo”
“Tena wewe mwana hizaya nilikuwa ninasubiria
uingize hilo domo lako lililo kosa haya kumbe wewe
ndio unawatuma hawa watoto ili walate jeuri si
ndio?”
“Hapana Zena ila heshima ni kitu cha bure na
tambua mujibu wako wa kazi ni upi ila si kuwatu-
kana watoto wawatu”
“Nenda kule………….Hanisi mkubwa wewe uliye na
Jogoo asiye wika anakazi ya kujikunyata ka-ma
mbwa jike anayesubiri kupandwa na mbwa dume”
“ZENA……… ZENA……..ZENA”
“Zena jina langu mtoto wa pwani niliye fundwa na
kujua jinsi ya kumkatikia yule anaye hitaji kuliko
wewe mwanaume suruali”
Machozi ya hasira taratibu yakaanza kunimwafika
huku mwili mzima ukitetemeka na kunifanya
nitazame chini na sikutaka wanafunzi waitadhimini
sura yangu ya hasira.Darasa zima limekaa kimya
wakimsikiliza Madam Zena anavyo ropoka maneno
machafu kiasi kwamba yanachafua masikio
“Wakisema wanaume watoke na wewe utatoka
mwanaume unaye kimbia vita na kufungia watu
milango kwa nje”
“ZENA FUNGA BAKULI LAKOOOO
“Heheee eti nifungea bakuli langu hata huyo anaye
nit*** haniambii nifungee bakulii lan-gu…..KANITA
NGAZEEE MWANAUME SURUALI WEEE”
Meza ya mwanafuzi aliyepo mbele yangu
nikainyanyua kwa hasira na kuirusha kwa nguvu na
kutua kwenye miguu ya Madam Z ena na
kumuangusha chini na kuwafanya wanafuni wote
kushangaa huku wakimtazama Madam Zena akipiga
kelele za kulalamika kuvunjwa mguu.Nikatoka
darasani kwa hasira na kwenda moja kwa moja
ofisini na kukaa kwenye kiti changu huku ninalia kwa
hasira na kuwafanya waalimu wengine kunishangaa
“Eddy unatatizo gani….?”
Sikumjibu mwalimu anaye niuliza swali na sikujua ni
mwalimu nani anaye niuliza swali hilo kutokana na
machozi mengi kunitawala machoni mwangu na
kingine nimeinama chini na kuegemzea sura yangu
mwenye meza huku machozi yakidondoka chini
sakafuni
“Eddy brother sema unatatizo gani…Umefiwa?”
Nikatingisha kichwa kuashiria kuwa sikufiwa na mtu
wa aina yoyote.Akaingia Madam Recho huku
akihema akionekana ametoka kukimbia na
kusimama katikati ya ofisi na kujifunga ushungi
wake kiunoni
“Jamani Eddy amemuua rafiki yangu Uwiiiiii huyu
mtu muuaji”
Waalimu wengine ikiwemo na mimi tukastushwa na
maneno ya Madam Recho na kila mwalimu akaanza
kuuliza huyo aliye uliwa yupo wapi
“Form Four A mimi leo asubuhi nimesema kuna
watu humu ndani ni majambazi ila mumezoea
kusema Ohhooo Recho mimi naongea sijui mimi
kinywa changu kipo wazi.Haya sasa nendeni
mukajionee maiti huko”
Waalimu wakaanza kutoka mmoja mmoja huku
wakikimbia kuelekea nje akiwemo Madam Re-cho
mwenyewe na nikabaiki na Madam Nyange ambaye
ni mama wa makomo.Akatoka kwenye kiti chake na
kuja kukaa karibu yangu
“Etii Eddy mwangu ni kweli umeua?”
“Mama yangu mimi hata sijui kama nimeua au laa?”
Nilizungumza huku nikilia na kumfanya Madam
Nyange kutoa kitambaa chake kwenye mfuko wa koti
alilo vaa na kunipa ili nijifute machozi
“Mmmmm sasa mwangu Eddy ilikuwaje kuwaje hadi
ikawa hivyo?”
“Mama Zena mchokozi”
Nikaanza kumuadisia Madam Nyange jinsi ilivyo
kuwa hadi nikachukau uamuzi wa kumua-dhibu
madam Zena na sikujua hali yake ipo vipi.Akaingia
Sir John huku akionekana kuchanga-nyikiwa huku
jasho likimwagika hadi limelowanisha shati
lake.Akaniangalia kwa jicho kali kisha akapiga hatua
za haraka na kunishika shiti langu na kuninyanyua
kisha akanipiga kwichwa kizito na kuniangusha chini
na kumfanya Madam Nyange kusimama na kumzuia
“Acha nimfunze adabu hawezi kumpiga demu wangu
na mimi nimuache na nitahakikisha uta-fungwa
wewe mbwa”
“John nakuomba utoke njee ”
“Mama siwezi kutoka kwani hajui ni kiasi gani
namaliza mshara wangu kwa kumtunza Zena alafu
leo kirahisi rahisi anakuja kunimpiga yeye kama
nani?”
“Sawa John ila nakuomba uende nje mwangu please
(tafadhali)”
“Tena ngoja niwapigie polisi waje wakubebe”
Sir John akatoka nje huku akiitoa simu yake mfukoni
na taratibu nikanyanyuka kutoka chini nilipoangukia
na kukaa juu ya kiti changu huku machozi yakizidi
kunimwagika
“Mwanangu ninakuomba uende zako nyumbani hali
imeshakuwa mbaya sawa baba”
“Hapana mama kama wanakuja kunikamata waje
wanikamatie hapa hapa kazini kwangu”
“EDDY Nakuomba nenda nyumbani sisi kama shule
hili tatizo tutajua tunalitatua vipi?”
“HAPANA MAMA”
Madam Nyange akakaa kimya huku huku
akinitazama kwa sura ya unyonge.Akaingia mkuu wa
shule na akanitazama kwa muda kisha akaniomba
nimfwate ofisini kwake.Nikanyanyuka na kuanza
kumfwata kwa nyuma mkuu wa shule na tukaingia
ofisini kwake na kukaa kwenye kiti kilichopo
pembeni ya meza yake
“Eddy hali ya Zena sio nzuri na hapa
ameshakimbizwa hospitalini hembu niambie ni kitu
gani kilicho kufanya umjeruhi Zena wakati
unatambua sheria ya kazi moja wapo ni ugomvi
haitajiki eneo la kazi sasa wewe umefanya nini?”
Nikakaa kimya nikimtazama mkuu wa shule na wala
sikujua nianzie wapi katika kulizungumzia swala lililo
nifanya nimpige Madam Zena.
“Eddy umeidhalilisha sana taaluma yetu ya ualimu
hivi unadhani kuna mwanafunzi atajenga heshima
kwako au kwa sisi waalimu ambao tunashindwa
kuzizuia hasira zetu na kupigana mbele zao.Na sote
tukisema tuwe ma JOHN CENA humu ndani si
tutauana kweli na shule itageuka uwanja wa Miereka
na….”
Kabla mkuu wa shule hajamalizia wakaingia askari
watatu walio valia sare za kipolisi na mmoja wao
akatoa kitambulisho na kujitambulisha huku nyuma
yao akiwepo Sir John
“Eddy mwenyewe ndio huyo hapo”
“John ni nini umefanya?”
“Mkuu huyu ni mwalifu na anastahili haki hii ya
kukamatwa wala musinilaumu katika hilo”
“Eddy tunakuomba tuongozane na wewe kwenda
kituoni tukahojiane na wewe mswali mawili matatu”
“Vijana wangu ninawaoba hili swala tulizungumze
kwa herufi kubwa kutokana hili swala lime-tokea
kihofisi basi nawaombeni tulizungumze”
Mkuu wa shule alizungumza huku akitoa wallet yake
iliyo jaa noti za elfu kumi kumi za kitanzania kiasi
kwamba wallet haifungi vizuri na akaanza kuhesabu
pesa kwa lengo la kuwapa polisi
“Mzee tunayaheshimu sana mawazo yako ila
hatujaja kuchukua pesa yako ila sisi tunamuhitaji
Eddy na kama hana kosa la aina yoyote basi
tutamuachia huru”
“Sawa ila mukitoka mumeongozana naye kidogo
inaweza ikaleta hofu kwa wanafunzi wetu ndio
maana ninawaomba tuyamalize humu humu
ofisini.Kumbukeni bila sisi nyinyi musinge vaa hizo
nguo zenu munazo ringia”
“Mzee sasa hayo ni matusi…..Asee wewe Eddy
nyanyuka jinsi unavyokaa hapa ndivyo unajiongezea
uzito wa kesi”
“Vijana wangu nawaombeni jamani tafadhali”
“Mkuu ngoja mimi niende ila Mngu mwenyewe ndio
atakaye nipigania wala usiwe na wasiwasi”
Nilizungumza huku nikijifuta machozi kwa kitambaa
alicho nipa Madam Nyange kisha nika-nyanyuka
taratibu na kuanza kupiga hatua za kutoka nje huku
askari wakifwa nyuma yan-gu.Nikakutana na
waalimu wengine wakabaki wamenitazama kwa sura
za huruma kasoro Ma-dam Recho aliye nizomea
kisiri siri.Wanafunzi wa kidato cha nne walipo niona
nimeongozana na maaskari wakatoka huku
wakinikimbilia wakiwa wanaliita jina langu na baadhi
yoa wakitokwa na machozi
“Sir Eddy hatuto soma hadi wewe uachiwe huru
kwani ukweli wote tunaujua sisi”
“Hapana wadogo zangu nyinyi someni kwani
kusoma ndio msingi wa maisha yenu.Hata ikitokea
nimefungwa sinto wasahau wadogo zangu”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika na
kuwafanya wanafunzi wa kike kuongeza vilio huku
kila mmoja akihitaji kunipa mkono wa kwaheri kabla
sijaingia ndaniya gari la polisi
“Sir kweli tutaandamana ili usifungwe…Wewe ndio
tunaye kuelea peke yako na hakuna mwen-gine
tunaye muelewa zaidi yako”
Mwanafunzi mmoja alizungumza kwa niamba ya
wezake huku machozi yakiwa yanamwagika.Askari
mmoja akanishaka suruali yangu na kutaka
kuninyanyua kwa nyuma huku akinihimiza nipende
kwenye gari.Wanafunzi wakaanza kumzomea askari
aliye nishika na ikambidi aniachie huku askari
wengine wakizishika bunduki zao vizuri kwani gari
lao lilianza kuzungukwa na wanafunzi hata wa
vidato wengine ambao hawakujua ni nini kinacho
endelea
“Wadogo zanugu muna nisikializa?”
“Ndio Sir Eddy!!!”
“Ninawaombeni murudi darasani siwezi kwenda jela
nawahakikishia kesho asubuhi tutakuwa pamoja
SAWA”
Nilizungumza na kupanda kwenye gari la polisi na
taratibu gari likaanza kuondoka endeo la shule na
kusababisha wanafunzi kuanza kulikimbiza kwa
nyuma huku wengine wakilirushia mawe na baadhi
ya wanafunzi wanao kuja shule na pikipiki na
baiskeli wakaanza kulifukuzia kwa nyuma gari la
polisi.Tukafika katika kituo cha polisi cha Mabawa
na nikaingizwa kwenye chumba cha mahojiano na
askari mmoja akaichukua simu yangu.Ila baada ya
muda kidogo nikasikia kelele za wanafunzi wakiimba
huku wakisema wanamtaka Mwalimu Eddy.Kelele
zikazidi kutawala kiasi kwamba ikapelekea askari
kuanza kupiga mabomo ya machozi ili kuwatawanya
wanafunzi
“Aisee hiyo miwanafunzi yako inakupenda eheee”
Askari mmoja aliniuliza huku akizungumza kwa
lafudhi ya kikuria na sikumjibu kitu zaidi ya kukaa
kimya.Ilaa baada ya muda sikusikia tena nyimbo za
wanafunzi wakiniimbia wakiwataka polisi waniachie
huru.Nikaendelea kukaa katika chumba nilicho
ingizwa huku kila askari akio-nekana hana haja na
mimi na kila mmoja aliendelea na shuguli zake.Mida
ya jioni nikaitwa na askari mmoja na kutoka nje ya
chumba nilichopo na kukutana na mwanamke nisiye
wahi kumuona katika maisha yangu
“Upo huru nenda zako”
Askari yule alizungumza huku akainipa simu yangu
na kujikuta nikiwa siamini kwa kitu kili-cho toke
kwani moja kwa moja nilijua maisha yangu ndio
yanaelekea ukingoni.Mwanamke niliye ambiwa
amenichukulia zamana akaniomb niongozane naye
hadi alipo lisimamisha gari lake na sikuwa mbishi
na nikamfwata huku njia nzima nikimshukuru kwa
kitu alicho nifanyia ila mweznangu hakunijibu kitu
chochote zaidi ya kutabasamu.Tukaingia kwenye
gari lake aina ya OPA na kukaa siti za mbele na
hatukuelekea sehemu yoyote zaidi ya gari kusimama
“Nakushukuru tena sana dada yangu”
“Eddy hauna haja ya kunishukuru nilitaka
nikuonyeshe jinsi nilivyo iongezea uwezo nyota yako
na lile lengo nililokambia nahitaji kukufanya mtu
mwenye dhamani daniani ndio linakwenda
kukamilika”
Sauti ya mwanamke huyo inafanana na sauti ya
Olvia Hitler ila umbo na sura havifanani naye kabisa
jambo lililo nifanya nianze kupata wasiwasi
“EDDY utataniogopa hadi lini?”
“Hapana sikuogopi”
“Eddy unajua sisi tuna uwezo mkubwa wa kukiona
kile kilichopo moyoni mwa mwanadamu na ndio
maana ninakuambia Eddy kuwa bado unaniogopa.Na
nimeamua kuja katika umbo ili na sura nyingine”
“Ila ni kwanini Olivia umeamua kunifanyia hivi
unavyo nifanyia?”
“Eddy huo ni mtihani wako wa kwanza na
umebakisha mitiani mingine sita ili itimu saba na
ukishafikia katika kiwango ninacho kihitaji mimi na
wala sinto kuambia ni lini mitihani hiyo itakamilika”
“Ila bado hujanijibu swali langu ni kwanini umeamua
kunifanyai hayo unayo nifanyia?”
Olvia Hitler hakunijibi kitu cha aina yoyote zaidi ya
kushuka kwenye gari na kuanza kuondoka
ikanilazimu na mimi kushuka kwenye gari ila
mwezangu akawahi kuvuka upande wa pili wa
barabara na kuniacha mimi nikiwa nimesimama
nikisubiria gari mbili zilizo ongozana zipite ndio
nivuke.Gari zikapiata na mimi nikavuka barabara cha
kushangaza sikuweza kumuona mwenzangu
ameelekea upande gani ikanibidi nirudi upande nilio
kuwepo na kilichozidi kunichanganya sikuikuta gari
tuliyo kuwepo.
Nikapata wazo la kwenda nyumbani kwa bibi niliye
kuwa ninaishi jirani naye,kwa woga nikao-gopa hata
kupanda bodaboda na ikanilazimu nianze kutembee
kutoka maeneo ya Mabawa hadi Chuda,nikaingia
kwenye duka moja na kurusha vocha kisha na
kuitoa simu yangu na kumpigia Hilda
“Shem mbona hadi sasa hivi haujarudi?’
“Kuna sehemu nitapitia hadi baadaye nitakuambia
uje unifwate?”
“Sawa ila upo salama kweli?”
“Ndio….kwanini unaniuliza hivyo?”
“Kwa sababu unazungumza kama unaumwa?”
“Kidogo sipo sawa kivile”
“Powa shem wangu kipenzi cha roho yanngu”
“Powa”
Nikakata simu na kuendelea na safari yangu na kwa
mbali kutoka nilipo hadi ilipo nyumba ya bibi
nikaona nje kumefungwa turubai huku watu walio
valia kanzu wakiwa wamekaa kwenye majamvi huku
ukimya ukiwa umetawala katika endeo hilo.Nikazidi
kuongeza mwendo huku akilini wazo la bibi kuwa
amefariki dunia likaanza kunitesa,Kabla sijafika
karibu na sehemu ilipo nyumba ya bibi nikastuka
mtu akinishika mkonno kwa nyuma huku akinivuta
kwa nguvu
ITAENDELA

No comments:

Post a Comment