Wednesday, November 23, 2016

NCHI YA WACHAWI 1


Kwa jina naitwa Israeli, lakini si yule mtoa roho za watu, hili ni jina ambalo linapatikana katika utaratibu wa maisha ya kila siku duniani.Nimezaliwa mwaka 1950, (kwa sasa 2010 ana miaka 60) wilayani Misungwi, mkoani Mwanza, ni mtoto wa kwanza katika familia yenye kujiweza kidogo kimaisha, ikiwa na watoto tisa, wote wanaume. Wazazi wangu (sasa marehemu) walikuwa wacha Mungu sana.Kama kweli kuna uhai baada ya kifo na wakayajua mambo yangu ya duniani, naamini nimewaumiza sana wazazi wangu.Kwa sasa naishi Mbagala, jijini Dar es Salaam na familia yangu yenye mke na watoto saba, wote wa kike. Mke wangu pia kwao ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto tisa, wote wanawake.Nimelazimika kusimulia mkasa huu wa kichawi baada ya watu wengi kusimulia mikasa yao wakidai waliwahi kuwa wachawi wakaacha kwa sababu mbalimbali ambazo wengine huzisema, wengine hufanya siri kubwa.Naweza kusema kwamba, karibu wote waliokuwa wakisimulia maisha yao ya kichawi na mikasa yake, hakuna hata mmoja aliyewahi kufikia hata robo ya maisha ya kichawi ya kwangu.Mimi niliishi maisha hayo kwa miaka kumi, na nilifika ‘levo' ya mbali, mfano kuwa Mkuu wa Kikundi na kusafiri sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya mikutano mikubwa ya kimataifa ya wachawi.Niliporudi, nilikuwa nakutana na wachawi wakubwa wa hapa nyumbani Tanzania na kuwapa maagizo ya utendaji katika makundi yao sehemu mbalimbali za nchi.Katika kipindi chote cha kuwa mchawi nilibaini mambo makubwa mawili, kwamba, maisha ya wachawi katika ulimwengu wao hayana tofauti yoyote na maisha ya watu wasio wachawi katika ulimwengu huu wa macho ya kawaida.Maandiko yanaposema kuwa, Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana ni kweli kabisa. Wachawi wanaamini kwamba, vitu visivyoonekana pia vilikuwa na siku sita katika uumbaji wa Mungu, siku ya saba akapumzika.Na hiyo ndiyo sera ya mchawi mara tu baada ya kujiunga katika kazi hiyo inayolaaniwa na wengi ulimwenguni kote.Kabla sijaenda mbele zaidi nataka kusema kuwa, kama kuna shughuli mbalimbali za binadamu zinazoonekana kwa macho ya kawaida duniani, pia kuna shughuli kama hizo hizo zisizoonekana kwa macho ya kawaida, lakini zinashirikisha wachawi na mambo yao. 

ALIVYO LITESA PENZI ^^^^^^ 7


mzee akaamua kunyosha mkono juu ili wale waliopo kwenye lile boti waweze kumwona na kumpa msaada.Kisha kufanya hivyo mzee John alijisemea moyoni "kama ni kufa wacha nikafie mbali" akazama tena majini huku akipiga mbizi kuelekea upande ilikokuwa ile meli,pamoja na jitihada zake nguvu nazo hazikuwai tena upande wake kwa kule kutokula chochote kwa muda mrefu na kuogelea umbali mrefu kulimfanya awe mchovu zaidi.Huku kwa wavuvi wenzake na mzee John hali ilikuwanitete kwani wote walikuwa wamekwisha poteza lakini upande walioelekea kulikuwa hakuna msaada wowote ule basi kwa matumaini hafifu na yenye harufu kali ya kifoi waliendelea kupiga mbizi ili kuitafuta nchi kavu.Wale watu waliokuwemo kwenye ile boti walifanikiwa kuona mkono wa mtu kwa mbali ambaye alikuwa akiomba msaada, wakasemezana wao kwa wao kisha kukubali kwenda kumwokoa yule mtu(mzee John).wakaendesha ile boti kwa kasi kubwa kuelekea mahali alipokuwa mzee John walipofika pale mmoja wao,ambaye alikuwa kiongozi wao alitoa amri"zamieni majini haraka kisha mwokoeni huyo" .wale jamaa waliruka haraka na kuingia majini huku wakiangaza huko na kule , baada ya dakika tano hivi kupita mzee John alikwisha okolewa, akiwa anahema kwa tabu sana hali iliyowapelekea wao kumpa huduma ya kwanza kisha kufanya hivyo waligeuza boti lao na kurudi kambini kwao.Wale wenzake na mzee John walijaribu kujiokoa lakini wapi nguvu ziliwaishia taratibu walianza kuelemea huku mmoja wao akinywa maji yale kwa kasi.Lo! maskini mvuvi yule alianza kuzama vivyo hivyo na mwenzake ambae tayari alikuwa amekwisha zama.Baada ya nusu saa maiti mbili zilionekana kuelea juu ya maji ,samaki nao hawakuwa nyuma kwani walishambulia zile maiti na kuacha mafuvu na mifupi vikishuka chini ya maji.Huku nyuma mkewe na mzee John alikwenda kuripoti polisi juu ya kupotea kwa mumewe,polisi wakaanza upelelezi wao mara baada ya kupokea taarifa hizo.Mzee John alipokea huduma ya kwanza iliyomfanya kuanza kujielewa.Baada ya kuangaza macho huku na huko akagundua kuwa yuko kwenye boti huku akiwa amezungukwa na watu asio wajua.Safari ya kuelekea kambini ili endelea hakuna mtu aliyekuwa akiongea chochote hali iliyomfanya mzee John kushituka kidogo akaamua kuuliza"samahani ninyi ni akina nani? akiwa na matumaini ya kupata jibu zuri mara alisikia sauti nzito ilioambatana na ukali"kimya""funga domo lako""itaendelea usikoseee...