STORY NA HADITHI ZA KUSISIMUA
Wednesday, November 23, 2016
ALIVYO LITESA PENZI ^^^^^^ 7
mzee akaamua kunyosha mkono juu ili wale waliopo kwenye lile boti waweze kumwona na kumpa msaada.Kisha kufanya hivyo mzee John alijisemea moyoni "kama ni kufa wacha nikafie mbali" akazama tena majini huku akipiga mbizi kuelekea upande ilikokuwa ile meli,pamoja na jitihada zake nguvu nazo hazikuwai tena upande wake kwa kule kutokula chochote kwa muda mrefu na kuogelea umbali mrefu kulimfanya awe mchovu zaidi.Huku kwa wavuvi wenzake na mzee John hali ilikuwanitete kwani wote walikuwa wamekwisha poteza lakini upande walioelekea kulikuwa hakuna msaada wowote ule basi kwa matumaini hafifu na yenye harufu kali ya kifoi waliendelea kupiga mbizi ili kuitafuta nchi kavu.Wale watu waliokuwemo kwenye ile boti walifanikiwa kuona mkono wa mtu kwa mbali ambaye alikuwa akiomba msaada, wakasemezana wao kwa wao kisha kukubali kwenda kumwokoa yule mtu(mzee John).wakaendesha ile boti kwa kasi kubwa kuelekea mahali alipokuwa mzee John walipofika pale mmoja wao,ambaye alikuwa kiongozi wao alitoa amri"zamieni majini haraka kisha mwokoeni huyo" .wale jamaa waliruka haraka na kuingia majini huku wakiangaza huko na kule , baada ya dakika tano hivi kupita mzee John alikwisha okolewa, akiwa anahema kwa tabu sana hali iliyowapelekea wao kumpa huduma ya kwanza kisha kufanya hivyo waligeuza boti lao na kurudi kambini kwao.Wale wenzake na mzee John walijaribu kujiokoa lakini wapi nguvu ziliwaishia taratibu walianza kuelemea huku mmoja wao akinywa maji yale kwa kasi.Lo! maskini mvuvi yule alianza kuzama vivyo hivyo na mwenzake ambae tayari alikuwa amekwisha zama.Baada ya nusu saa maiti mbili zilionekana kuelea juu ya maji ,samaki nao hawakuwa nyuma kwani walishambulia zile maiti na kuacha mafuvu na mifupi vikishuka chini ya maji.Huku nyuma mkewe na mzee John alikwenda kuripoti polisi juu ya kupotea kwa mumewe,polisi wakaanza upelelezi wao mara baada ya kupokea taarifa hizo.Mzee John alipokea huduma ya kwanza iliyomfanya kuanza kujielewa.Baada ya kuangaza macho huku na huko akagundua kuwa yuko kwenye boti huku akiwa amezungukwa na watu asio wajua.Safari ya kuelekea kambini ili endelea hakuna mtu aliyekuwa akiongea chochote hali iliyomfanya mzee John kushituka kidogo akaamua kuuliza"samahani ninyi ni akina nani? akiwa na matumaini ya kupata jibu zuri mara alisikia sauti nzito ilioambatana na ukali"kimya""funga domo lako""itaendelea usikoseee...
Saturday, September 17, 2016
tangulia kuzimu
Alivunga kwa hili na lile kabla hayajashusha pumzi ndefu na kusema “Oke, hayo tuyaache yashamwagika hayazoleki tena. Vipi kuhusu Saadan, anasema bado anakupenda licha ya yote yaliyotokea yuko tayari pia kukuoa na kuwalea watoto wako iwapo utakubali kwenda kuishi nae Oman. Unasemaje Nasra mwanangu?”
Nasra akaachia tabasamu dogo, akageuka na kumtazama Saadan, alikuwa kijana mzuri sana ingawa kwake hakuwa na mvuto kama ule aliokuwa nao Promota Halfan.
“Naweza nikakubali baba ikiwa tu atanitekelezea masuala fulani fulani”
“Good!” Alwatan Dafu akaruka kwa furaha “Masuala gani?”
“Moja nataka umfutie kesi Promota Halfan! Najua unahusika!”
“What?”
“Eeeh! Hilo la kwanza la pili baada ya kumfutia kesi nataka umuombe radhi kwa kumpiga na kumdhalilisha siku ile ya fainali pale Diamond Jubilee. Aidha nataka umuheshimu na umuhakikishie kuwa hutambughudhi tena na tena umtambue kama mkweo aliyepita na baba wa watoto wangu!”
“Mpuuzi!” Alwatan Dafu akanguruma, sharubu zikicheza cheza kwa hasira. Mikono pia ikimcheza cheza. Akaendelea kuongea povu likimtoka mdomoni.
“Nasema mpuuzi!! Una wazimu… una wazimu… unawazimu! Sababu ulizotoa sijui masharti hakuna zima hata moja. Nasema utaolewa tu, upende usipende!”
“Bila kutimiza hayo siolewi!” Alikuwa Nasra kwa kiburi.
“Huwezi kunichezea kama umejizaa mwenyewe sasa utanitambua! Hasira zikamzidi Alwatan Dafu akakunja mikono ya kanzu na kumjongelea mwanae huku akitetemeka kwa hasira.
Akamuinua pale kitandani na kumtandika vibao viwili vya nguvu. Nasra akaanza kulia, watoto wake pia wakaanza kulia! Hii haikumfanya Alwatan Dafu asimuinue zaidi na kumkunja vizuri kwa kutumia “Blouse” yake. Mkono wake wenye nguvu ukitua katika shingo la Nasra, Sadaan akamwahi na kumzuia.
Nasra akapata nafasi ya kuinuka, akawaifadhi wanae vizuri pasipo kukijali kilio chao halafu akamfuata baba yake, akipiga kelele zilizochanganyikana na kilio.
“Saadan! Muache, muache aniue, father kill me, kill me please! Maisha gani haya! Nilishachoka muache aniue ndio niue tu!!” akajitahidi kumnasua lakini Saadan akawa imara.
“Saadan!” Dafu akafoka akitweta “Acha nimfundishe hawezi kuniendesha anavyotaka. Hajakauka huyu kwamba nitashindwa kumkunja, mimi ni baba yale lazima aniheshimu, asikilize ninataka nini niache nimtandike!” povu zilizidi kutoka katika madomo wa Alwatan Dafu.
“Saadan, leave him! Mwache aniue!” Nasra anaendelea kupiga kelele akimfuata baba yake. Hamad! Alwatan Dafu akaponyoka mikononi mwa Saadan na kumfuata Nasra.
Nasra nae akamfuata!
Wakakutana katikati. Alwatan Dafu alimdunda Nasra kama ngoma! Makelele ya Saadan ndiyo yaliyowaita walinzi na wahudumu wa hospitali ile ambao walifika wanamundoa Alwatan Dafu toka katika shingo ya Nasra.
Huku akikohoa na kushika shingo lake kwa maumivu, Nasra aliendelea kumfuata baba yake na kuomba watu waliomshika mzee wake wamuache amuue.
Mama Nasra ambaye alikuwa amerudi hima kufuatia makelele yaliyopigwa na Saadan alishangaa kuikuta hali aliyoikuta, akamvuta Nasra na kumshika kwa nguvu.
“Mama niache! Niache baba akaniue, ndio nataka anitoe roho niepukane na hili balaa. Inakuwaje anifanye na kunigeuza vile apendavyo, vile atakavyo? Vile ajisikiavyo? Mie mwanasesere? Mie mtoto wa bandia? Niache mama, niache!
Mie ni binadamu kamili kama wengine. Mwenye uhuru, mwenye haki, mwenye uwezo wa kuamua! Vipi ayaingilie mamuzi yangu? Vipi auingilie utashi wangu, vipi aninyanyase? Niache akaniue nitoweke!”
“Hasira hazisaidii mwanangu!”
“Potelea mbali!” Nasra akataka aondoke tena lakini karipio la nguvu toka kwa mama yake aliyemvuta kwa nguvu ndio lililomrudisha.
“Mimi kama mama yako nasema acha, acha kabisa!” akafoka. Nasra akamsikiliza mama yake akarudi na kumkumbatia akiongeza kasi ya kilio.
“Mama! Nakupenda mama! Lakini roho inaniuma mama. Moyo wa subira sasa unaambulia zilizooza baada ya mbivu, uvumilivu wake umeuponza. Roho inauma mamaaah!”
Akazidisha kilio mara dufu. Mama yake akamfariji kwa kumkumbatia huku akumpigapiga mgongoni kwa vikofi vidogo vya upendo. Akamwambia.
“Najua! Najua kama inauma! Vuta subira zaidi itapoa na utasahahu!”
Walinzi waliomshika Alwatan Dafu sasa waliweza kumdhibiti vizuri na kupata ahueni baada ya mama Nasra kumdhibiti Nasra.
Alwatan Dafu akapozwa kiutu uzima hata akakubali kutoka nje. Saadan akampakia kwenye gari waliyokuja nayo na kuondoka. Alipomfikisha kwake, akamtaka apumzike kwa muda halafu yeye akarudi hospitali alikolazwa Nasra lengo lake lilikuwa moja tu kusikia Nasra anasema nini.
Naam! Toka atoke Oman, karibuni miezi miwili nyuma alikuwa hajabahatika kupata nafasi ya kuongea na Nasra kwa tuo. Kila alipokuwa akijiandaa kuongea nae yalitokea haya na yale ambayo yaliharibu na pengine kuvuruga maandalizi hayo.
Hakika! Alimkuta Nasra akijiandaa kupumzika, mama yake nae alikuwa pembeni akamsalimu na kumsalimia Nasra kisha akaketi pembeni yao kabla ya hajaanza kuwaangalia mmoja baada ya mwingine kwa zamu.
“Samahani mama,” Akaanza kwa upole na heshima na kuendelea
“Inawezekana pengine nafanya makosa kukuita hivyo pasi ya idhini yako wala ya Nasra. Lakini madhali umemzaa Nasra ambaye tunakaribia kulinganalingana, sioni kwa nini usiwe mama yangu, sioni! Hata hivyo natanguliza radhi za dhati kama muono wangu ni opofu!” akatua kuvuta pumzi.
“Bila samahani Saadan, wewe ni mwanangu kwa kila hali kuwa huru sijui unasemaje?” akajibiwa
“Unajua nilikuja huku Afrika na hususani hapa Tanzania kwa ajili ya kumuoa Nasra. Na haki ya nani nilimpenda Nasra toka nilipomuona mara ya kwanza katika picha.
Na siku nilipokuja kumtia machoni ‘live’ kwa mara ya kwanza pale jukwaani Diamond Jubilee, upendo wangu kwake ukaongezeka mara dufu mpaka sasa ninampenda kuliko tafsiri halisi ya neno hilo…”
“Saadan!!” Nasra akaingilia kwa karaha “Natumai hukuja hapa kumueleza mama yangu jinsi unavyonipenda sawa?” Saadan alipokubali kwa kutikisa kichwa Nasra akahitimisha kwa kusema “Basi mashairi achana nayo, mueleze lililokuleta!”
“Usihamaki Nasra! Ninachofanya ni kujenga msingi wa mazungumzo na labda maelezo yangu ili aweze kunielewa vizuri au ni makosa kufanya hivyo?”
“Yeah! Inawezekana!” Alikuwa Nasra tena
“Nasra hebu muache mwenzio aongee kwanza!” Mama Nasra akaingilia. Nasra akanyamaza kwa shingo upande.
“Naomba msamaha tena endapo nimekosea ninachotaka kusema ni kwamba toka nimefika hapa nimeshuhudia vingi na mengi, lakini sijapata nafasi moja muhimu nayo ni kuongea na Nasra.
Nilipofika hapa siku moja kabla ya shindano, niliambiwa nisiongee na Nasra kwani naweza kumchanganya kiasi cha kumfanya afanye vibaya. Niliheshimu.
Mashindano yakafanyika, akafanya vizuri lakini yaliyotokea ukingoni mwa shindano sote tunafahamu na kwa vile Nasra alipoteza fahamu kwa siku kadhaa, kila wakati nimekuwa nikifika hapa na kukosa nafasi ya kuongea nae na hali ya kuwa ni nusu mfu!
Sikukata tamaa nimesubiri kwa mapenzi mazito na uvumilivu mkubwa mpaka leo hii muumba alipoleta Baraka zake. Lakini mara nyingine tena yametokea ya kutokea ambayo sote tumeyaona. Ingawa Alwatani Dafu ananipa matumaini lakini mimi siyo mtoto wa kudanganywa na pipi.
Ndiyo sababu nikatangulia kuomba radhi mama, naomba uniruhusu niongee na Nasra faragha ili nijue msimamo wake kwangu ukoje! Ili niweze kujua kama nastahili kusuka au kunyoa! Ni hilo tu.”
Mama Nasra akamgeukia mwanae na kumtazama kama anayemuuliza “Unasemaje’. Nasra akabetua mabega na midomo kama nayesema sitaki au sijui. Mama Nasra akatabasamu na kumgeukia Saadan!
“Bila samahani mwanangu. Ninaweza tu kukupa nafasi nzuri ya kuongea na Nasra, usifadhaike. Usijali, usijali hata kidogo” akamjibu akachukua baadhi ya nepi za watoto na kwenda kuzifua nje.
Nasra akamuangalia Saadan na kuketi vizuri kitandani. Akamnyanyua mtoto wake mmoja aliyekuwa analia na kumnyonyesha halafu akamuuliza Saadan kwa kiingereza.
“Enhe! Unataka kuongea nini na mimi?”
“Mengi tu Nasra!” Saadan akajibu kwa kiingereza pia na kuendelea “Nadhani ingekuwa vizuri kama tungeanza kwa kuongelea habari za ndoa yetu. Sio siri mimi ninakupenda sana, tena sana sijui wewe kwangu?”
“Una maana gani Saadan?”
“Unataka kuniambia kwamba hujui kilichonitoa Oman kunileta hapa?
“Naweza kusikia, kwamba umekuja kufunga ndoa na mimi si ndo hivyo?”
“Yah! Uko sahihi”
“Lakini tayari umemkuta Nasra akiwa mjamzito na mbaya zaidi kajifungua Diamond Jubilee mbele ya halaiki ya watu tena watoto mapacha! Hufikirii kwamba huyu Nasra unayetaka kumuoa leo alikuwa Malaya, mshenzi wa tabia na kiruka njia ambaye anaweza kukuambukiza hata Ukimwi?”
Saadan akatulia tuli pasipo kujibu. Nasra akaendelea
“Haya, umeshuhudia ugomvi baina ya Nasra na baba yake. Hivi hufikirii kama Nasra anaweza kuwa mbishi na kupigana na baba yake mzazi, aliyemzaa, akamlea na kumosomesha; vipi baba wa Saadan! Atamsalimisha kweli? Na kama hatomsalimisha, huo ukoo wa Saadan utamuelewaje Nasra?” Akatulia tena, bado Saadan alikuwa kimya.
“Hiyo tisa! Kumi nina watoto hawa tena mapacha, hawa bado wanahitaji uangalizi wa karibu wa mimi mama yao, hasa ukizingatia uduni na udhaifu wa afya zao. Utawaeleza nini wanaukoo wenu ambao watahoji juu ya watoto hawa?!
Naomba ufikirie vizuri uamuzi wako Saadan, mie nafikiri sifa zangu chafu zinanifanya nikose sifa za kuwa mke mwema kwako. Najua unanipenda, tena unanipenda sana! Hilo nalifahamu fika.
Na tena ninashukuru mno kwa msaada wako wa hali na mali ulioutoa kwangu toka pale jukwaani mpaka hapa Aga Khan hospiatal! Kitendo cha kujitolea kuwasaidia wanangu wasiokuhusu ndewe wala sikio, kinanifanya nikose cha kukulipa zaidi ya kusema Asante, Mungu atakulipa zaidi!” Nasra akahitimisha.
Saadan akatabasamu na kusema “Nasra mimi ndiye ninakwenda kuishi na wewe siyo baba, mama, kaka, dada, ndugu na wala wanaukoo wangu. Mimi nina akili, uelewa na ufahamu mzuri siwezi kukulaumu kwa yaliyotokea kwa vile tayari nimeshajua ulikuwa ukiishi maisha ya namna gani. Siwezi kukulaumu kabisa.
Shukrani zako nimezipokea, lakini sio kweli kwamba huna cha kunilipa. Upendo wako kwangu ni malipo tosha, malipo yatakayouacha Moyo wangu ukiwa umesuuzika vilivyo.
Bila shaka pia, baba na mama washakwambia kuwa mimi nipo tayari kuishi na wewe na watoto wako tena nitawalea kwa upendo na mapenzi yote kama baba yao mzazi, kama baba aliyefundwa vyema kulea. Tafadhali Nasra nipokee tuishi pamoja!”
“Maneno yako mazuri na hayachoshi masikioni Saadan, lakini ingawa sina hakika, najijua fika kwamba mimi ni mcheshi. Yeah! Wazazi marafiki na jamaa wananiambia hivyo, hata waalimu waliniambia hivyo hivyo.
Nina hakika ukaidi wako wa kujitia kunijali mimi kuliko ndugu zako, utawafanya ndugu zako wajenge nidhamu ya woga wakijitia kuuheshimu uamuzi wako wa kuoa msichana Malaya mwenye watoto wawili wasio wako.
Lakini chuki zao kwangu hazitajificha, zitaonekana dhahiri bin shahiri! Kitu kinachonifanya niishi pasipo ushirikiano wa kati yangu na wanaukoo wenzako.
Na mimi siwezi kuishi kwa amani wakati fika sielewani na wifi, sielewani na shemeji na baba mkwe au mama mkwe siwezi! Nahitaji kila mtu anizoee, tutaniane, tucheke na kufurahi ndio maana nikakwambia ufikirie uamuzi wako tena, fikiria tafadhali!”
“Niufikirie vipi Nasra? Inatosha kusema ninakupenda na kukuhitaji kuliko unavyoweza kufikiria. Sijui kwa nini unashindwa kunielewa, ndugu zangu sio wakatili kama unavyowafikiria na labda watakuchukia si unaweza kuniambia?”
“No! utakuwa mwanzo wa kukuchonganisha na ndugu zako. Hiki ni kitu kingine ambacho sikipendi daima dumu nitataka kuona mkiishi kwa upendo, amani, furaha, kama mlivyokuwa mkiishi baada ya mimi kufika!”
Saadan akamtazama Nasra na kuyafikia majibu yake, zilikuwa hoja za uhakika ambazo zingemgharimu muda mwingi kuziweka sawa ili kuondoa mashaka kwa Nasra, akajikuta akishusha pumzi za kukata tamaa na kusema.
“Sasa unataka kuniambia nini? Kwamba hunipendi na hutaki kuolewa na mimi?”
Ikawa zamu ya Nasra kumtazama Saadan kwa muda kabla hajayarudisha macho chini, kwa ujumla Saadan alikuwa amekata tamaa. Akaachia tabasamu dogo na kumuonea huruma.
“Sikiliza Saadan! Nikikwambia nakupenda, upendo kama huo ulionao wewe kwangu ninakuongopea! Baba wa watoto hawa ndiye haswa aliyeushika moyo wangu. Hata hivyo juhudi zako zimenifanya nigundue ni namna gani unavyonipenda.
***SAADAN anaelezea hisia zake zote kwa NASRA lakini NASRA anamuwaza baba wa watoto wake…..
****Mzee Dafu analazimisha mwanaye aolewe na SADAAN nini kitajiri..
ITAENDELEA

Friday, August 26, 2016
MIRATHI YA KAKA 2...
‘Nitapona kweli leo?’ Huu ni mfano wa baadhi ya maswali yaliyokuwa yanayosumbua akili yangu kwa wakati huo. Nilikosa majibu ya maswali yangu, nikaishia kujisemea Mungu yupo.
Sasa endelea....
Tetemeko lilikoma ghafla, pakawa shwari tena, lakini giza lilikuwa lipo palepale. Mvua kubwa ilianza kunyesha, mwanga na miungurumo ya radi nilizidi kuvishuhudia.
Nilibaki nimeduwaa baada ya kugundua kuwa pale nilipokuwa silowi licha ya mvua kubwa kuendelea kunyesha. Hakuna hata tone moja la maji lililokuwa likinifikia utadhani nilikuwa chini ya mwamvuli, nilizidi kuchanganyikiwa.
Hata kwa chini maji hayakunigusa hivyo nyayo zangu zilikuwa kavu. Lakini mvua nilikuwa naishuhudia ikinyesha, tena ni bonge la mvua.
Nilibaini kuwa kumbe nilikuwa nipo juu ya kilima baada ya mwanga wa radi kumulika. Lakini hapakuwa hata na mwamvuli juu yangu licha ya kutoangukiwa na tone hata moja.
Mara niliona kitu kama shuka jeupe kikishuka kutoka angani. Nilikisubiri kwa hamu kitu hicho ili nione ni nini kitatokea.
Woga ulianza kupungua. Siyo kwa kuwa nilikuwa nimeyazoea mazingira; la hasha! Ulipungua kutokana na kukata tamaa nikijua kuwa kuokoka kwangu ni asilimia 0.0025. Nilijipa uhakika wa kupoteza uhai endapo kudura za Mwenyezi Mungu zisingechukua nafasi.
Kitu hicho kilizidi kuteremka taratibu, tena kilikuwa wima mithili ya kitambaa cha sinema. Japokuwa giza lilikuwa limetanda angani kote, kitu hicho kiling’ara na niliweza kuushuhudia mng’ao wake. Shauku ya kutaka kuona kitakachotokea ilizidi kunishika, moyo wa woga haukuwepo tena kwa wakati huo.
Kitu hicho kilianguka chini, moshi mwingi niliushuhudia kilipokuwa kimeangukia. Moshi uliendelea kutoka mahali hapo lakini kitu hicho mfano wa shuka kilikuwa hakionekani tena.
Kufumba na kufumbua niliwaona watu katikati ya moshi huo, nikashindwa kujua idadi yao kamili kwa sababu walikuwa wanatembeatembea bila ya kutulia. Licha ya moshi mwingi kutanda eneo hilo, watu hawa walionekana ‘live’ tena bila chenga.
Nilizidi kuchanganyikiwa nilipoanza kuwatambua baadhi yao, kilichokuwa kinanishangaza ni kwamba kila niliyemtambua alikuwa kashatangulia mbele ya haki tukamzika, yaani namaanisha alishakufa kitambo.
Itaendelea......
SITOSAHAU SIKU HII
Ni siku nyingi kidogo, mwaka 1980, lakini ni tukio ambalo liliniuma sana. Ilikuwa vigumu sana kulisahau na lilinifanya nijiulize, inakuwaje Mungu anakuwa mkatili kiasi kile. Lakini bila shaka ilikuwa ni wakati ule wa ufahamu mdogo. Hivi sasa ninafahamu mengi na hasa baada ya kujifunza maarifa haya ya utambuzi.
Ilikuwa ni mwaka 1980 nikiwa nasafiri kutokea Dar es salaam kwenda Arusha. Sijui ilikuwaje, lakini ilitokea. Tuliondoka Dar es salaam saa 12.30 jioni. Wakati ule mabasi yalikuwa yakisafiri jioni na usiku, sio kama siku hizi.
Nilikuwa ninakwenda Arusha kwenye usaili kwa ajili ya ajira, nikiwa ndio kwanza nimemaliza kidato cha nne. Niliajiriwa moja kwa moja serikalini, kwani siku zile ajira zilikuwa ni za kumwaga. Hata hivyo
sikuridhishwa na kazi niliyokuwa nafanya, hivyo niliomba kazi kwenye kampuni moja kule Arusha na niliitwa kwa usaili.
Tulifika mji unaoitwa Korogwe ambao wakati ule ulikuwa ndio mji maarufu kwa hoteli zake katika barabara yote ya Segera hadi Moshi na Arusha. Tulipofika Korogwe basi letu lilisimama kwa ajili ya abiria kupata chakula. Niliingia kwenye hoteli moja ambayo nakumbuka hadi leo kwamba ilikuwa ikiitwa Bamboo. Niliagiza chakula na kula haraka kutokana na muda mfupi wa kula uliotolewa na wenye basi la TTBS ambalo ndilo nililosafiri nalo.
Wakati wa kulipa ndipo niliposhangaa na kuogopa. Niliingiza mkono mifukoni na kukuta kwamba sikuwa na hela. Nilianza kubabaika na mwenye hoteli alisema hawezi kukubali ujinga huo, "Abiria wengine wahuni bwana, anakula na kujifanya kaibiwa, ukikubaliana nao kila siku hasara tu" Mwenye hoteli alisema kwa kudhamiria hasa.
Kulizuka zogo kubwa, huku mwenye hoteli akisema ni lazima anipeleke polisi. Ni kweli alimtuma mmoja wa watumishi wake kwenda kituo cha polisi ili nishughulikiwe……
Hapo Hotelini kulikuwa na bwana mmoja aliyekuwa amekaa pembeni na mkewe na watoto wao wakila. Yule bwana alipoona vile alimtuma mhudumu mmoja aniite. Niliondoka pale kaunta nilipokuwa nabembeleza na kuja kwa yule bwana.
Alikuwa ni kijana mtu mzima kidogo, mwenye miaka kama 50 hivi. Nilimsalimia na aliitikia, nilimsalimia mkewe pia. Yule bwana aliniuliza kisa cha vurugu ile na nilimsimulia. Aliniuliza sasa huko Arusha ningeishi vipi wakati wa usaili wakati nimeibiwa fedha zote na ningerudi vipi Dar. Nilimwambia nilikuwa napanga namna ya kurudi Dar, kama huko polisi ningeaminika.
Kama mzaha vile yule bwana aliniambia kuwa angenipa fedha za kutumia huko Arusha na nikirudi Dar nimrudishie fedha zake. Nakumbuka alinipa shilingi 90 kwa ahadi kwamba nikirudi Dar nimpelekee fedha zake ofisini kwake. Alinielekeza ofisini kwake, mtaa wa Nkuruma na kuniambia kuwa ameamua kunisaidia kwa sababu kila binadamu anahitaji msaada wa mwingine na maisha haya ni mzunguko. Nilimshukuru na kuondoka kukimbilia basini. Basi lilikuwa linanisubiri mimi tu. Nilipanda ndani ya basi na abiria wengine walinipa pole. Tuliondoka Korogwe, lakini haikuchukua muda basi letu lilipata tatizo la pancha ya gurudumu moja la mbele. Ilibidi tuegeshe pembeni ili litengenezwe. Baada ya matengenezo, tuliondoka kuendelea na safari yetu.
Karibu na mji wa Same kwenye saa saba usiku, basi letu lilisimama ghafla. Abiria walisimama ndani ya basi na kulizuka aina ya kusukumana. Huko nje kulikuwa na ajali. Abiria tulishuka haraka na wengine huko chini walishaanza kupiga mayowe, hasa wanawake. Niliposhuka niliona gari ndogo nyeusi ikiwa imebondeka sana na hapo kando kulikuwa na maiti wawili.
Nilijua ni maiti kwa sababu walikuwa wamefunikwa gubigubi. Halafu kulikuwa na katoto kalikokuwa kanalia sana kakiwa kamefungwa kanga kichwani. Tumwahishe huyu mtoto hapo Same hospitali ameumia, ingawa sio sana. Nilikatazama kale katoto ka kiume kenye umri wa miaka kama mitatu. Kalikuwa kameumie kwenye paji la uso, lakini kalikuwa hai. Bila shaka wale walikuwa ni wazazi wake, kalikuwa yatima tayari. Machozi yalinitoka.
Baada ya kupata msaada na askari wa usalama barabarani kuchukua maiti wale tulipanda basini kuendelea na safari yetu. Kale katoto kalichukuliwa na jamaa fulani waliokuwa na Land Rover ya serikali kukimbizwa hospitalini. Ndani ya Basi mazungumzo yalikuwa ni kuhusu ajali ile tu, hadi tunafika Arusha. Tulichelewa sana kufika Arusha kwani tulifika kwenye saa tano asubuhi, badala ya saa mbili .
Nililala kwenye hoteli rahisi na kufanya usaili kesho yake. Ni hiyo kesho, baada ya usaili niliponunua gazeti ambapo nilipata mshtuko mkubwa ajabu. Kumbe wale watu wawili waliokufa kwenye ajali ile ya Same walikuwa ni yule bwana aliyenisaidia hela na mkewe. Yule mtoto wao ndiye aliyeokoka. Niligundua hilo baada ya kusoma jina lake na jina la kampuni aliponiambia nimpelekee fedha zake nikirudi Dar, pamoja na picha yake, mke na mtoto. Nililia sana, kama mtoto.
Nillishindwa kujua ni kwa nini afe. Nilijiuliza ni nani sasa angemlea mtoto yule? Yalikuwa ni maswali yasiyo na majibu na pengine maswali ya kijinga pia.
Nilijua kwamba nilikuwa na deni, deni la shilingi tisini. Kwa wakati ule shilingi tisini zilikuwa ni sawa na shilingi laki moja za sasa.
Kwa mara ya kwanza sasa nilijiuliza ni kwa nini marehemu yule aliniamini nakuamua kunipa fedha zile. Sikupata jibu.
Nilikata kipande kile cha gazeti la kingereza kilichokuwa na habari ile. Nilichukuwa kipande hicho na kukiweka kwenye Diary yangu. Deni, Ningelipa vipi deni la watu? Nilijikuta nikipiga magoti na kuomba mungu anipe uwezo wa kuja kulilipa deni la mtu yule mwema kwa njia yoyote. 'Mungu naomba uje uniwezeshe kulilipa deni la marehemu kwa sura na namna ujuavyo wewe. Nataka kulilipa deni hili ili nami niwe nimemfanyia jambo marehemu,' niliomba. Nilirejea Dar siku hiyo hiyo.Kwa sababu ya mambo mengi na hasa baada ya matokeo ya usaili ule kuwa mbaya kwangu, nilijikuta nikiwa na mambo mengi na kusahau haraka sana kuhusu mtu yule aliyenisaidia mbaye ni marehemu. Nilifanikiwa hata hivyo kupata nafasi ya kusoma Chuo cha Saruji na baadae chuo cha ufundi na hatimaye nilibahatika kwenda nchini Uingereza. Mwaka 1992 nilianza shughuli zangu.
Ilikuwa ni mwaka 1995 nikiwa ofisini kwangu pale lilipokuwa jengo Nasaco ambalo liliungua mwaka 1996, ambapo lilijengwa upya na kubadilishwa jina na kuitwa Water Front. Nikiwa nafanya kazi zangu niliambiwa na sekratari wangu kwamba kulikuwa na kijana aliyekuwa anataka kuniona. Nilimuuliza ni kijana gani, akasema hamjui. Nilimwambia amruhusu aingie. Kijana huyo aliingia ofisini. Alikuwa ni kijana mdogo wa umri miaka kama 17 au 18 hivi, mweupe mrefu kidogo. Alikuwa amevaa bora liende , yaani hovyohovyo huku afya yake ikiwa hairidhishi sana.
Nilimkaribisha ilimradi basi tu, kwani niliona atanipotezea bure muda wangu. Ni lazima niwe mkweli kwamba sikuwa mtu mwenye huruma sana na nilikuwa naamini sana katika watu wenye pesa au majina. Nilimuuliza, “nikusaidie nini kijana na ukifanya haraka nitashukuru maana nina kikao baada ya muda mfupi”. Nilisema na sikuwa na kikao chochote , lakini nilitaka tu aondoke haraka.
“Samahani mzee, nilikuwa na shida…..nimefukuzwa shule na sina tena mtu wakunisaidia kwa sababu …..nime….niko ….kidato cha pili na hivyo tu natafuta tu kama atatokea mtu……..
Nilimkatisha. “Sikiliza kijana. Kama huna jambo lingine la kusema, ni bora ukaniacha nifanye kazi. Hivi unafikiri kama nikiamua kumsaidia kila mtu aliyefukuzwa shule si nitarudi kwetu kwa miguu! Nenda Wizara ya Elimu waambie……Kwanza wazazi wako wanafanya kitu gani, kwa nini washindwe …..Kwa nini walikupeleka shule ya kulipia kama hawana uwezo, wanataka sifa?”
“Hapana wazazi wangu walikufa na ninasoma shule ya serikali. Nimekosa mahitaji ya msingi na nauli ya kwendea shule. Nasoma shule ya Kwiro, Morogoro. Shangazi ndiye anayenisomesha, naye ana kansa na hivi sasa hata kazi hafanyi….,” Alianza kulia. Huruma fulani ilinijia na nilijiambia, kama ni nauli tu na matumizi, kwa nini nisiwe mwema, angalau kwa mara moja tu. “Baba na mama walifariki lini?” Niliuliza nikijua kwamba, watakuwa wamekufa kwa ukimwi, maana kipindi kile ndipo fasheni ya ukimwi ilipoanza, ambapo kila anayekufa huhesabiwa kwamba kafa kwa ukimwi.
“Walikufa kwa ajali nilipokuwa mdogo sana, nilipokuwa na miaka mitatu. Ndio shangazi yangu akanichukua na kunilea hadi sasa anakufa kwa kansa.” Yule kijana alilia zaidi. Naomba nikwambie wewe msomaji unayesoma hapa kwamba, kuna nguvu fulani na sasa naamini kwamba ziko nyingi ambazo huwa zinaongoza maisha yetu bila sisi kujua.
Kitu fulani kilinipiga akilini paaa! Nilijikuta namuuliza yuel kijana. “Kwa nini umeamua kuja kwangu, ni nani alikuelekeza hapa na wazazi wako walikufa mwaka gani na wapi?”
Yule kijana alisema, “Nimeona nijaribu tu kwa mtu yeyote ambaye anaweza kunisaidia, na ndio nimejikuta nikiingia hapa, sijui……..sikutumwa na mtu. Wazazi wangu walikufa mwaka 1979 huko Same na mimi wanasema nilikuwa kwenye ajali, nikaokoka. Niliumia tu hapa.” Alishika kwenye kovu juu ya paji lake la uso.
Nilihisi kitu fulani kikipanda tumboni na kuja kifuani halafi niliona kama vile nimebanwa na kushindwa kupumua. “Baba yako alikuwa anaitwa nani?” “Alikuwa anaitwa Siame….Cosmas Siame….” Niliinuka ghafla hadi yule kijana alishtuka . Nilikwenda kwenye kabati langu mle ofisini na kuchakura kwenye droo moja na kutoka na diary. Mikono ikinitetemeka, nilitoa kipande cha gazeti ndani ya diary hiyo, nilichokuwa nimekihifadhi.
“Ndio alikuwa anaitwa Cosmas Siame. Huyu ni mtoto wake, ni yule mtoto aliyenusurika.” Nilinong’ona. Nilijikuta nikipiga magoti na kusali. “Mungu, wewe ni mweza na hakuna kinachokushinda. Nimeamini baba kwamba kila jema tunalofanya ni akiba yetu ya kesho na kesho hiyo huanzia hapa duniani.” Halafu nillinyamaza na kulia sana. Nililia kwa furaha na ugunduzi wa nguvu zinazomgusa binadamu kwa kila analofanya.
Nilisimama nikiwa nimesawajika kabisa. Nilihisi kuwa mtu mwingine kabisa. Nilimfuata yule kijana na kumkumbatia huku nikiwa bado ninalia. “Mimi ni baba yako mdogo, ndiye nitakyekulea sasa. Ni zamu yangu sasa kukulea hadi mwisho” Naye alilia bila kujua sababu na alikuwa amechanganyikiwa kabisa. Nilirudi kwenye kiti na kumsimulia kilichotokea miaka 17 iliyopita.
Tuliondoka hapo na kwenda kumwona shangazi yake Ubungo, eneo la maziwa ambako alikuwa amepanga chumba. Kutokana na hali yake nilimhamishia kwangu, baada ya kumsimulia kilichotokea. Huyo dada yake Cosmas alifurahi sana hadi akashindwa kuzungumza kwa saa nzima. Alifariki hata hivyo mwaka mmoja baadae, lakini akiwa ameridhika sana.
Kijana Siame alisoma na kumaliza Chuo Kikuu na hivi sasa yuko nchini Australia anakofanya kazi. Ukweli ni kwamba ni mwanangu kabisa sasa. Naamini huko waliko Mbinguni wazazi wake wanafurahia kile walichokipanda miaka mingisana nyuma. Lakini nami najiuliza bado. Ilikuwaje Cosmas akanipa msaada ule? Halafu najiuliza ni kitu gani kilimvuta mwanae Siame hadi ofisini kwangu akizipita ofisi nyingine zote? Nataka nikuambie, usiwe mbishi sana bila sababu, kuna nguvu za ziada zinazoongoza matokeo maishani mwetu.

NIMEKOSA NIN
Alfajiri na mapema niliamka. Sikuamka kwa bahati mbaya muda huo bali ilikuwa ndiyo kawaida yangu kila siku. Nilikuwa nikiamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kwenda katika mihangaiko yangu ya kila siku.
Ingawa siku hiyo nilikuwa kwenye mtoka kisha nikachelewa sana kurudi nyumbani, sikuwa na budi ya kujidamka asubuhi na mapema ili niende kazini.
Baada ya kupiga mswaki niliingia maliwatoni kujiswafi. Nilipomaliza nilirudi chumbani kwangu, nikauramba kama ilivyokuwa ada kila nilipokuwa naelekea kazini.
Nilichukua suruali yangu niliyokuwa nimevaa jana yake nilipokuwa kazini ili nichukue pochi iliyokuwa kwenye mfuko wa suruali hiyo kwani humo ndiyo kulikuwa na nauli yangu ya kunipeleka kazini na kunirudisha nyumbani.
“Umeiona pochi yangu mama Chris?” Nilimuuliza mke wangu aliyekuwa kajilaza kitandani kwa wakati huo.
“Hata sijaiona, kwani ulikuwa umeiweka wapi?” Aliuliza.
“Nakumbuka jana nimeenda nayo kazini, lakini nimeangalia kwenye suruali niliyokuwa nimevaa sijaiona.”
“Mh! Sasa itakuwa wapi?”
“Kama vipi achana nayo kwa sasa, acha niende kazini nikirudi nitakuja niitafute vizuri! Cha kufanya sasa hivi nipe shilingi elfu kumi kwa ajili ya nauli.” Niimwambia mke wangu naye akainuka na kunichukulia kwenye droo ya kitanda kisha akanipatia.
Nilimuaga mke wangu kwa kumbusu kwenye paji la uso kisha nikamalizia kwa mwanangu kipenzi aliyekuwa bado kalala.
“Kila la heri mume wangu, nakutakia kazi njema!” Yalikuwa ni maneno ya mke wangu kipenzi mama Chris, maneno ambayo alikuwa akiniambia kila siku nikiwa naelekea kazini.
“Asante mama, na wewe nakutakia siku njema, utamsalimia mwanangu Chris atakapoamka.” Nilijibu huku nikichana chana nywele zangu huku nikijiangalia kwenye kioo kikubwa kilichokuwepo kwenye meza ya kujirembea iliyokuwemo humo chumbani.
Nilipoanza kuondoka mama Chris akanishika mkono,
“Ngoja kwanza baba wewe!” Alitamka maneno yale wakati akiuvuta mkono wangu!
“Nini tena mama?” Nilihoji kwa lugha ya kubembeleza nikidhani kuwa labda mama Chris anataka mambo yetu yale ya mchezo wa kikubwa, maana katika kumbukumbu zangu usiku huo timu zote zilikuwa kambi kwani mwenzangu alikuwa katika sherehe zake za kila mwezi.
“Hii tai haijakaa vizuri mume wangu, angalia na hii kola ya shati lako shingoni ilivyokaa shaghala baghala, utaenda unachekwa njia nzima!” Aliongea wakati akinirekebisha huku tabasamu lake mwanana akilitoa.
“Nitachekwa mimi au utachekwa wewe mke wangu maana umeshindwa kunikagua wakati natoka!”
“Mimi sitachekwa sababu sitakuwepo huko.” Aliongea mke wangu huku akihamia kwenye tai kuiweka sawa.
Alipomaliza kuyaweka sawa mavazi yangu nilimkumbatia tena kwa mara nyingine na kumpiga mabusu motomoto kisha nikatoka zangu. Nilienda mpaka stendi kugombania daladala, si unajua tena usafiri wetu wa huku Bongo.
Sikuchelewa kupata gari, nikapanda na kwenda kushukia posta mpya kisha nikaanza kutembea kwa miguu kuelekea ofisi yetu ilipokuwa.
Nilipofika ofisini nilipigwa na butwaa baada ya kuwakuta watu wamejazana. Kwa haraka haraka nikaanza kuhisi kuwa kuna tukio kubwa ambalo lilikuwa limetokea. Watu walikuwa wameuzunguka mlango huku polisi wakiwa wanarandaranda.
Maswali mia mia yakaanza kuzunguka katika akili yangu bila kupata majibu. Kwa kuwa nilikuwa tayari nipo kwenye tukio lenyewe, nilipiga moyo konde na kujiambia kuwa muda si mrefu nitakijua kilichojili.
“Halafu linaonekana ni tukio kubwa sana, yaani mpaka polisi wamekuja!” Nilijiwazia huku nikitembea kwa tahadhari kuelekea ofisini.
ITAENDELEA........
Tuesday, August 23, 2016
TANGA RAHA
‘MAMA NINAKUOMBA UNIPE BARAKA ZAKO ILI
NIWEZE KUMUOKOA BABA YANGU’
‘NAKURUHUSU KWA MOYO MMOJA NA MWANANGU
NITAKUPA MSAADA WA CHOCHOTE UTAKACHO
KIHITAJI HATA NUSU YA NGUVU ZANGU NITAKUPA
ILI BABA YAKO AWE HURU KWANI BADO
NINAMPENDA SNA’
‘MAMA NIMEDHAMIRIA KUIANZISHA DUNIA MPYA NA
YENYE KILA AINA YA NGUVU ZITAKAZO IPINGA
MAMLAKA TULIYOPO JUU YETU’
ENDELEA
“Mazungumzo kati ya Hitlaer na mama yake ambaye
ni Janet yaliendelea kwa usiri mkubwa hu-ku mama
yake akimfundisha mbinu ambazo zitamsaidia
mwanae katika kuikamilisha kazi ya kumuokoa baba
yake.Hitler alijipanda vizuri na kutokana ni mjukuu
wa miongoni mwa Malaika wakubwa mbinguni
aliweza kutumia kigezo hicho kushuka duniani bila
ya kuhojiwa maswali mengi na walinzi wanao linda
dunia ambayo ipo katika hali mbaya ya kuuguzwa
moto.

Subscribe to:
Posts (Atom)